News

Posted On: Mar, 02 2023

TTB YAWANOA WADAU WA UTALII WA KITAMADUNI KANDA YA KUSINI

News Images

Wakati serikali ikiendelea kuboresha miundombinu ya barabara na viwanja vya ndege, Bodi ya utalii nchini TTB imeanza kutoa mafunzo kwa wadau wa utalii wa kitamaduni Kanda ya kusini ili kuwandaa kuitumia fursa hiyo kukuza biashara zao.

Mafunzo hayo yanafanyika mkoani Iringa yakihusisha wadau kutoka mikoa iliyopo kanda ya kusini kupitia Mradi wa Kuboresha Usimamizi wa Maliasili na Kukuza Utalii Kusini (REGROW).

Akizungumza katika mafunzo hayo afisa kutoka bodi ya utalii nyanda za juu kusini HOZA MBURA alisema lengo la mafunzo hayo nikuhakikisha huduma za utalii wakitamaduni zinatolewa ipasavyo kwa wageni wanaotembelea maeneo yakihistoria ili kusaidia kukuza pato la mwananchi na taifa kwa ujumla .

HOZA Alisema utalii wa kitamaduni ni utalii ambao ni tofauti na utalii wa wanyamapori ,kwahiyo wameona ni vyema kuanza kuwaandaa wadau hao namna yakutafuta masoko ili kuutangaza utalii kimataifa.

“Bodi ya utalii TTB tumekuwa tukitangaza utalii wa kitamaduni kama zao jipya kwa watalii, kwahiyo tumeamua kufanya mafunzo haya kwa wadau ili kuwasaidia kutoa huduma ipasavyo kwa watalii pindi wanapotembeea maeneo yao ,tunawafundisha mbinu mbalimbali ikiwemo namna ya kujiuza katika masoko ya utalii duniani ili wapote watalii wengi na waweze kuvutia utalii wa kitamaduni hapa nchini”alisema HOZA

Kwa upande wake ofisa utalii mkuu kutoka mamlaka ya usimamizi wa wanyamapori nchini, Elirehema Matulo alisema kutoka na jitihada za serikali zakuutangaza utalii ni lazima jamii katika maeneo mbalimbali iandaliwe kwakupatiwa elimu ya namna ya kuandaa mazao mbalimbali ya utalii wakitamaduni

ELIREHEMA aliongeza kuwa ili utalii huo wakitamaduni uweze kujulikana katika kanda ya kusini ni vyema wadau hao kuwa tayari kujifunza kutoka kanda ambazo zimefanikiwa ikiwemo kaskazini

“tumeona kule kaskazini utalii huu wakitamaduni unafanya vizuri kwahiyo wadau wakusini wana eneo la kujifunza kwakushirikiana kwakubadilishana uzoefu katika kuunganishiana fursa mbalimbali za biashara ili waweze kufanya vizuri, kwahiyo kwasasa kusini nako kumefunguka jamii zimehamasika kwa ajili yakuanzisha utalii huu ili kuhakikisha kwamba wanajipatia kipato kupitia utalii”alisema

David jan ni mhadhiri mwandamizi kutoka chuo kikuu cha Dar es salaam alisema utalii wakitamaduni haujashika kasi kutokana na jamii nyingi kuacha kuenzi mila na desturi zao

Mhadhiri huyo Alisema kabila la wamaasai limefanikiwa kutokana na kuishi katika mila zao na kupelekea kuvutia watalii wengi wanaokuja kutembelea vivutio vya utalii nchini.

nao baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo akiwemo FARQU ISMAIL na AMOS ASAJILE walisema mafunzo hayo yamewasaidia kuelewa kwa kina kuhusu utalii wa kitamaduni ukilinganisha na hapo awali,kwani walijua utalii wa kitamaduni ni ngoma za asili pekee.

haya yanajiri wakati serikali ya awamu ya sita chini ya Rais DR. SAMIA SULUHU HASSAN iliagiza kila mkoa kufanya matamasha ya utamaduni ili kutangaza mila na desturi za watanzania ili kuongeza wigo mpana wa wageni wanaofika nchini kutalii kukaa muda mrefu kujifunza ili kufikia malengo ya nchi yakupata watalii million tano kwa mwaka ifikapo mwaka 2025