News
TTB YATUMIA FURSA YA “ THE Z-SUMMIT KUTANGAZA VIVUTIO VYA UTALII VYA TANZANIA
Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) ni Miongoni mwa Taasisi za Serikali zinazoshiriki katika Mkutano wa Kimataifa wa Sekta ya Utalii “The Z-SUMMIT” pamoja na Maonesho yanayohusisha wadau wa utalii. Mkutano huu wa kwanza kufanyika viziwani Zanzibar umefunguliwa rasmi na Rais wa Zanzibar, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi una lengo la kuwaunganisha wadau wa sekta ya utalii na wawekezaji wa ndani, Afrika Mashariki na kimataifa.
Mkutano huu wa siku mbili unafanyika katika Hotel ya Golden Tulip kuanzia tarehe 23 & 24, Feb, 2023 ambapo Wadau kutoka nchi mbalimbali wanashiriki.Bodi ya Utalii Tanzania imetumia fursa ya mkutano na maonesho hayo kutangaza vivutio vya utalii vya Tanzania hususani vivutio vya ukanda wa kusini mwa Tanzania. Bodi pia imeweza kutoa elimu ya jinsi jamii inavoweza kufaidiaka na kujiongezea kipato kwa kuanzisha vikundi vya utalii wa kiutamaduni, ambapo watalii wataweza kujifunza mila na desturi za makabila ya Tanzania.