News

Posted On: Mar, 12 2023

​MKURUGENZI MKUU TTB AWATAKA WATUMISHI KUTEKELEZA MAJUKUMU YAO KWA KUSHIRIKIANA

News Images

Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Bw. Damasi Joseph Mfugale amefanya kikao na watumishi wa TTB kwa lengo la kujitambulisha kwa watumishi na kutoa dira ya namna watakavyokuwa wanatekeleza majukumu yao ya kila siku. Hiki ni kikao chake cha kwanza tangu kuteuliwa kwake na Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Bw. Mfugale amewasisitizia watumishi wa TTB kufanya kazi kwa kushirikiana na kuzingatia muda. Alisisitiza kuwa, huua ndio uwe utamaduni wao kwa kazi zote watakazopangiwa, Kinyume na hapo mtumishi atakuwa amekwenda kinyume na makubaliano na maelekezo ya kikao.

Mkutano huo wa watafanyakazi wote uliwajumuisha pia watumishi wa Ofisi za TTB kanda kwa njia ya mtandao. Watumishi kwa kauli moja tarehe 14 Februari,2023 waliahidi kumpatia ushirikiano wote na kutekeleza maagizo na maelekezo aliyoyatoa, Kikao kilifanyika katika ofisi za TTB Makao Makuu jijini Dar es Salaam.